“TOROKA UJE” BAA YA WIKI SHINDANO LA “FANYAKWELI KIWANJANI”

Dar es salaam, 16 Mei 2015 Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani limeanza kutimua vumbi kwa kuzishindanisha baa mbalimbali za jiji la Dar es salaam kama ilivyokua imetangazwa hapo awali.

Mapema jioni ya jana, wadhamini wanaoendesha shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake cha Tusker Lager wakishirikiana na kituo cha redio E-fm, walifunga kambi katika baa hiyo iliyopo Kimara-Korogwe jijini Dar na kuporomosha burudani ya nguvu huku wakitoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa kinywaji cha Tusker waliojumuika kwenye hafla hiyo.

Kikubwa kilichowavutia zaidi wateja waliofika kwenye baa hiyo ni huduma nzuri ya vinywaji, vyakula, fursa ya kutuma salamu moja kwa moja kupitia redio E-fm sambamba na zawadi kutoka SBL kama Tisheti na bia za bure za Tusker zilizotolewa kwa wateja hao na mtangazaji wa E-fm Bw. Gadner kwa staili mpya iliyojulikana kama Mupe Mureke.

Mmoja kati ya wateja wa baa hiyo aliyejishindia Tisheti na bia za bure katika hafla hiyo  kwa jina la Wema Usiri (30) akizungumzia baa hiyo alisema… “Nimefurahi sana baada ya kusikia “Toroka uje” imekua baa ya kwanza kushinda promosheni hii ya Fanyakweli Kiwanjani kiukweli inastahili”. Bi Usiri aliongeza kuwa sababu kubwa inayoifanya baa hiyo kupendwa sana ni kutokana na huduma zao nzuri hasa upande wa vyakula, vinywaji sambamba na burudani za kila aina kama muziki wa bendi unaopigwa kila ijumaa na jumamosi mahali hapo. Wengine walioibuka na zawadi za bia na Tisheti ni Bwana na Bi Lema, Romana Mwikombe na Anneth Kimaro.

Kwa upande wake Meneja Vipoozeo na mwonekano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Baraka Mandara aliyemwakilisha Meneja Chapa wa Tusker alianza kwa kuwashukuru wananchi wa Kimara-Korogwe na wapenzi wote wa Kinywaji cha Tusker waliofika kwenye hafla hiyo ili kusherehekea kwa pamoja ushindi wa baa hiyo. “Lengo kuu la Kampeni hii ni kuziwezesha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli kwa kuzitambulisha kwa wananchi ambao tunaamini kutokana na sapoti yao baa hizi zitaongeza vipato.”

Bw. Mandara aliendelea kwa kusema kuwa “Toroka uje” ndio baa ya kwanza kufungua promosheni hiyo na kuwasisitiza wapenzi wa Kinywaji cha Tusker kuendelea kupiga kura kwa wingi ili kuziwezesha baa za mitaa yao kushinda.

Promosheni hii ya “FanyaKweli Kiwanjani” ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker “FanyaKweli” ambapo itadumu kwa takriban muda wa wiki tano huku zaidi ya baa 50 za jiji la Dar es salaam zikipewa fursa ya kushiriki kwenye shindano hilo. Kila wiki kutakua na mshindi mmoja kati ya baa 10 zitazokuwa kwenye kinyang’anyiro. Ili kuiwezesha baa ya mtaa unaoishi tembelea baa hiyo kisha burudika na kinywaji cha Tusker na piga picha nyingi uwezavyo na uipendekeze baa hiyo kwa kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za Tusker au kusikiliza kipindi cha ubaoni kinachorushwa na redio E-fm kati ya saa tisa hadi moja usiku ndani ya siku za juma kwa maelezo zaidi.

H Kimati
hkimati@abstrat.co.tz